Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584629

Habari Kuu of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samia ashusha rungu zito kwa Lukuvi, 'hatagombea uspika!'

William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Ardhi William Lukuvi, aliyekuwa Waziri wa Ardhi

Baada ya Rais Samia kufanya mabadiliko katika Braza la Mawaziri, yapo mengi yaliyoibuka juu ya wale waliotemwa katika uteuzi wa Mawaziri hasa aliyekua Waziri wa Ardhi, William Lukuvi kutolewa katika Baraza la Mawaziri jipya lilioundwa na Kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Akizungumza wakati wa hafla ya uuapishwaji wa Mawaziri, Manaibu Waziri, Majaji na wenyeviti wa Tume mbalimbali, Rais Samia mapema leo Januari 10, 2022 amesema kuwa kiongozi huyo atapangiwa majukumu mapya ambayo atayatangaza siku za karibuni.

Rais Samia amesema kuwa kuna minongono mingi inayoendelea katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na jumbe za maandishi zilizotengenezwa kwa nia ya kumchafua kiongozi huyo ambaye amemtaja kama mchapakazi imara aliyefanya makubwa ndani ya Wizara ya Ardhi.

Amesema kuwa siku si nyingi atatangaza majukumu mapya ya kiongozi huyo huku akisawazisha hali ya hewa kwa kuwakata kilimi wale wote wanaoendelea uvumi kuwa Lukuvi amejipanga kuwania nafasi ya uspika kuwa jambo hilo halipona kuwa kiongozi huyo anayo kazi maalum.

"Kuna wale waliosema bora Lukuvi katoka, niwambie tu kuwa hajatoka, na ale wanaosema anagombania uspika niseme tu kuwa hata gombania uspika! huyu ana kazi na mimi na siku si yingi nitaitangaza"