Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583942

Habari Kuu of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samia atamba kwa kutoa ajira 14,000 kwa vijana

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Serikali imesema kuwa kwa kipindi cha miezi tisa iliyopita imeweza kutoa ajira 14,000 kwa vijana nchini kwa malengo ya kuondoa utegemezi na kukuza uchui wa taifa kwa ujumla.

Haya yamebainishwa na Rais Samia wakati wa Maandamano ya maadhimisho ya miaka 58 ya mapinduzi ya Zanzibar mapema Januari 07,2021.

“Katika kipindi cha miezi 9 ya serikali ya awamu ya sita, serikali imetoa ajira zipatazo 14,000 na serikali itaendelea kuangalia fursa mbalimbali zitakazotoa ajira kwa vijana wetu.

“Serikali yetu tunajua tatizo la ajira, tutalifanyia kazi, tunatambua tatizo hilo kwa vijana.

“Vijana pia wanakabiliwa na ukosefu wa ufundi stadi, wanamaliza kusoma wanakaa na cheti kusubiri ajira za serikali.

“Vijana wengi tukimaliza kusoma tunasubiri ajira, hatutumii fursa,” - Rais Samia Hassan Suluhu akishiriki maandamano ya Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar, leo Ijumaa.