Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560398

Habari za Afya of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Saratani ya kizazi bado tishio Tanzania

Saratani ya kizazi bado tishio Tanzania Saratani ya kizazi bado tishio Tanzania

SARATANI ya shingo ya kizazi imetajwa kuwa tishio kwa wanawake wa Mtwara, licha ya huduma ya vipimo vya awali kutolewa bure

Kwa kujibu wa takwimu zilizotolewa na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi ya Baba, Mama na Mtoto mkoani Mtwara, Rosalia Arope, zinaonyesha kuwa kuna asilimia 16 ya akina mama ambao wamegunduliwa kuwa na tatizo la saratani ya mlango wa kizazi kwa kipindi cha miezi sita tu.

Arope, amesema kuwa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, wakina mama 7,783 walichunguzwa na kati yao 100 walibainika kuwa na viashiria vya saratani na baada kufanyiwa uchunguzi zaidi asilimia 16 walingundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi huku 43 wakionyesha kuwa na dalili kubwa za ugonjwa huo hatari.

Arope, amefafanua kuwa wanawake walio kwenye hatari zaidi ni wale wenye wapenzi zaidi ya mmoja kutokana na virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi kubebwa na wanaume.

"Kundi lingineni ni wakina mama wale walioanza tendo la kujamiana wakiwa na umri mdogo, walio zaa wakiwa na umri mdogo, walioathirika na magonjwa ya ngono, watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama ukimwi, wanao zaa mara kwa mara, uzito mkubwa na kutofanya mazoezi na dalili zake zinaweza kujionyesha kuanzia miaka 10 hadi 15," amesema.

Amesema lengo la Mkoa kwa mwaka ni kuwachunguza wakina mama 117,000 sawa na wakina 9,789 kila mwezi lakini Mkoa unashindwa kufikia lengo kutokana na mwamko mdogo wa wanajitokeza kupima na kufikia angalau asilimia 13 ya maadhimio.