Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554608

Habari za Afya of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: Jamii Forums

Saudi Arabia haipokei mahujaji waliopata chanjo ya Sinovac!

Chanjo ya Sinovac Chanjo ya Sinovac

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui ametoa muongozo kwa wanaotaka kwenda Hijja na wamechoma Chanjo ya Sinovac kurudia kuchoma tena Chanjo ya Johnson & Johnson kwakuwa Saudi Arabia haiitambui Chanjo ya Sinovac.

Sinovac imeanza kutolewa Zanzibar mnamo July 23, 2021, imepitishwa na Shirika la Afya Duniani, lakini Saudi Arabia inazitambua chanjo aina ya Astrazeneca, Pfizer na Johnson & Johnson

Tanzania Bara ilipata dozi 1,504,000 za Johnson & Johnson ambapo 4.5% ilibidi iende Zanzibar. Waziri Mazrui ameomba Waislamu wanaotaka kushiriki Umrah wapewe kipaumbele