Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573835

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sekta ya kilimo yapumlia mashine, ajira zashuka kwa 5%

Sekta ya kilimo yapumlia mashine, ajira zashuka kwa 5% Sekta ya kilimo yapumlia mashine, ajira zashuka kwa 5%

Ajira zinazopatikana katika sekta ya kilimo nchini zinatajwa kupungua kwa asilimia 5.1 katika kipindi cha miaka sita kutoka 2015 hadi 2021.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa matokeo ya utafti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka 2020/2021 ambao umelenga katika kufahamu viashiria vya soko la ajira nchini ambao huisaidia Serikali kupanga bajeti yake.

Akizindua utafti huo Leo Novemba 24, 2021, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa ajira katika sekta hiyo zimepungua kutoka asilimia 67.4 za mwaka 2014 hadi asilimia 61.1 kwa mwaka 2020/2021.

"Hapa tuna upungufu wa asilimia 5.1 na hawa waliopungua wamehamia katika uwekezaji mwingine kama vile wa viwanda...." Amesema Waziri Mkuu.

Aidha ameongeza kusema kuwa Serikali imejipanga katika kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta hiyo ili kuwavutia watu wengi kuwekeza kwani kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa taifa.

Matokeo ya utafti huo yanawasilishwa visiwani Zanzibar mbele ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hussein Mwinyi huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa Mgeni Rasmi.