Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544651

Habari za michezo of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Senzo awapa  matumaini Yanga

Senzo awapa   matumaini Yanga Senzo awapa  matumaini Yanga

SIKU moja baada ya wanachama wa klabu ya Yanga kupitisha kwa asilimia 100 rasimu ya mabadiliko ya Katiba na muundo wa uendeshaji wa klabu hiyo, mshauri wa masuala hayo, Senzo Mazingiza amesema kazi kubwa iliyokuwa mbele yao ni kuhakikisha wanatimiza yale waliyoahidi.

Yanga imepania kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo ili kuachana na utegemezi wa fedha kutoka mfukoni kwa mtu mmoja na kujitegemea kwa mfumo wa uwekezaji na kampuni.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Senzo alisema sasa ni wajibu wao kama kamati kuhakikisha wanayatimiza yale yote ambayo waliahidi ili kuwapa furaha wanachama na mashabiki wa Yanga.

Mshauri huyo alisema huu ndio wakati sahihi wa kuanza kuyafanyia kazi masuala hayo, kila kiongozi kwa wakati wake anatakiwa kuwajibika kwa kupigania maendeleo ya klabu hiyo sababu endapo watafanikisha waliyokusudia ana amina timu hiyo itakuwa ya kupigiwa mfano.

Alisema pamoja na yote ana imani kubwa na uongozi wa Mwenyekiti, Dk Mshindo Msolla kwamba kama ilivyokuwa mwanzo wakati wanaanza mchakato huo, watapambana na kuhakikisha malengo yao yanafanikiwa na kuifanya Yanga timu ya kipekee kuanzia ndani na nje ya Tanzania.

Senzo alisema uendeshwaji wa mpira umebadilika duniani kote na mabadiliko ambayo wameyafanya yatabadilisha mpira wa Tanzania na kuvishawishi vilabu vingi vya Tanzania na nchi za jirani kuiga uendeshwaji huo.

Kiongozi huyo amewashukuru wanachama wa Yanga kwa kuonesha imani kubwa kwa kamati iliyofanikisha jambo hilo na yeye ameahidi kuwapambania hadi siku ya mwisho ili kuona mchakato huo unakamilika na Yanga inaendeshwa kisasa kama ilivyo baadhi ya klabu Afrika na Ulaya.