Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 551884

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali Kupitia upya Sera zilizopitwa na wakati

Jenista Muhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na  Walemavu Jenista Muhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema serikali ipo katika mchakato wa kupitia upya sera zilizopitwa na wakati ikiwemo za mwaka 1992 ambazo hazijafanyiwa mapitio ili ziweze kuendana na wakati na mazingira yaliyopo sasa.

Waziri Mhagama ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za serikali ambapo amesema zipo baadhi ya sera ambazo ni za muda mrefu na zimepitwa na wakati.

Ameongeza kusema kuwa maboresho haya yatasaidia kutoa mwanya kwa vijana kupata nafasi zitakazowainua kiuchumi kwa maendeleo ya taifa.