Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552400

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali: "Tozo za Miamala" haziwezi kufutwa

Tozo za Miamala ya simu Tozo za Miamala ya simu

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa Tozo ya Mshikamano haiwezi kufutwa, kwakuwa imewekwa kwa mujibu wa sheria ya bunge, na kueelza kuwa serikali haijakaa kimya kuhusu suala hilo bali wananchi wawe watulivu.

Amefafanua kuwa kinachoangaliwa kwa sasa ni kanuni na kuwa kamati ikishamaliza kuzipitia watatoa majibu kaa ilivyo agizwa na Rais Samia.

"Tozo ile iliwekwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge, haiwezi kufutwa, kinachoangaliwa sasa ni zie kanuni ambazo Waziri ana mamlaka ya kuzitengeza ziende zikatoze, zikikamilika watanzania watapewa majibu, si kama Serikali imekaa kimya, kuna kazi inafanyika ili tutoe majawabu ambavyo Rais ameagiza, lakini tusivunje Sheria ya Bunge ambayo imeagiza tozo hii, na tozo hii ni kwa ajili ya maendleo ya wananchi"

Ameeleza kuhusu umuhimu wa Kodi hiyo, kuwa ni kwa ajili ya kuharakisha maendeleo kwenye Jamii, ameongeza kuwa mbinu zakutafta kodi hazijakosekana ila kilichofanyika ni kukusanya maoni ya wadau ambao ni watanzania.

"Mbinu hazikukosekana, hili la kuweka tozo za miamala, limetokana na maoni ya wadau , hao hao watanzania, kwamba wigo wa kodi ni mchache, kila siku kukusanya kwenye bia bia, Serikali imesikia na miongoni mwa maoni ni kukusanya kodi kupitia miamala ya simu"