Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 20Article 572935

Habari Kuu of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali haijazuia maandamano- Prof Kabudi

Serikali haijazuia maandamano Serikali haijazuia maandamano

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi amesema Serikali haijazuia maandamano na mikutano ya kisiasa haijazuia nchini isipokuwa wanaandaa utaratibu rafiki utakaotumika pasipo kuvunua sheria za nchi.

Kabudi amesema kuwa inatambua umuhimu wa mikutano ya siasa na pindi utaratibu utakapokamilika watatangaza mfumo mpya.

“Maandamano na mikutano ya kisiasa haijazuiwa nchini ila inaratibiwa na imewekewa utaratibu. Ndio maana ninasema haijazuiwa. Hakuna jambo linalofanyika bila utaratibu. Tunasoma sura ya pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuhusu haki za binadamu bila kusoma ibara ya 30 iliyoweka mipaka ya wewe kufaidi uhuru wako,” amesema Kabudi.

Aidha, ametaja mipaka iliyowekwa kuwa ni mtu kutoingilia uhuru na haki ya mwingine, maagizo ya umma, usalama na afya.

Waziri huyo amesema mipaka hiyo imewekwa pia katika uhuru wa kuabudu na imani ambapo mtu anatakiwa kuifuata anapotumia uhuru wake.

Ameongeza kusema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka ambao kuepusha ghasia kwa watu wengine na mipaka hiyo haipo Tanzania pekee bali mataifa mengine pia.

Amefafanua kwa kusema kuwa Tanzania ni nchi pekee Kusini mwa Jangwa la Sahara yenye Sheria ya Vyama vya Siasa baada ya kurejea katika mfumo wa vyama vingi ambayo imeweka wajibu na majukumu huku vihakikishiwa ruzuku kwa vile vinavyoshinda ubunge na udiwani inayotokana na kodi za wananchi.

Kuhusu maandamano, amesema lazima kuwe na utaratibu ikiwamo kujulikana kwa mahali na siku ya kuyafanya.