Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 10Article 556522

Habari Kuu of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali imeruhusu uvunaji wa Mamba

Serikali kuruhusu uvuvi wa mamba baada ya utafiti Serikali kuruhusu uvuvi wa mamba baada ya utafiti

Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema inafatilia idadi ya mamba waliopo katika Mito inayopatikana katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Morogoro kabla ya kutoa vibali vya uvuaji wa mamb hao.

Akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Morogoro Kusini, Innocent Kalogerism, Waziri wa Maliasili, Damas Ndumbaro amesema kuwa wizara hiyo itatoa vibali kwa waliowasilisha maombi ya kuvua mamba pindi Wizara hiyo itakapo pata idadi kamili ya mamba hao.

""Ikiwa tutagundua kuwa idadi ya mamba katika eneo hilo ni ndogo, itatusaidia kutambua mamba wanaoshambulia watu na na hapo bsi tutaruhusu wavuliwe ..."amesema Waziri huyo.

Hatua hii imefikiwa kufuatia kukithiri kwa matukio ya Mmamba kushambulia wananchi wanaoishi katika maeneo jirani na vilipo vyanzo hivyo vya maji.