Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 05Article 555400

Habari Kuu of Sunday, 5 September 2021

Chanzo: ippmedia.com

Serikali imesitisha leseni ya "Raia Mwema" kwa siku 30

Leseni gazeti la Raia mwema yasitishwa kwa siku 30 Leseni gazeti la Raia mwema yasitishwa kwa siku 30

MKURUGENZI wa Idara ya Huduma za Habari Gerson Msigwa, amesitisha kwa muda wa siku 30 leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la Raia Mwema kuanzia kesho Septemba 6, 2021

Uamuzi wa kusitisha leseni ya gazeti hilo unatokana na mwenendo na mtindo wa uandishi wa habari na makala ambao kwa kiasi kikubwa unakiuka misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa na makala ambao kwa kiasi kikubwaunakiuka misingiya maadili ya taaluma ya habari kwa kufanya upotoshaji wa mara kwamara wa taarifa na uchochezi wa bayana, taarifa imeeleza.

Taarifa hiyo imesema kuwa kwa vitendo hivyo gazeti limekiuka masharti ya leseni iliyopewa jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaweza kuhatarisha usalama wa nchi kwa kuleta chuki miongoni wa jamii na vileile kuwafanya wanachi wachukie serikali na viongozi wake.