Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552187

Diasporian News of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Serikali imetangaza fursa za uwekezaji "Uchumi wa Blue" Zanzibar

Fursa kwa wawekaji Uchumi wa bluu kufunguliwa Zanzibar Fursa kwa wawekaji Uchumi wa bluu kufunguliwa Zanzibar

Wajumbe wa sekta binafsi na wadau wa visiwa Zanzibar wametakiwa kuchangamkia fursa ya uchumi wa Blue kupitia mpango nwa sekta binafsi kwa Umma (PPP) ili kuunga mkono serikali kukamilisha lengo lake la kujenga uchumi imara.

Wito huo umetolewa kwenye kikao kazi cha kujadili fursa za uwekezaji zanzibar katika matumizi bora ya rasilimali za bahari kwa ajili ya kuimarisha au kukuza uchumi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mawaziri wawili. Waziri wa kazi, Uchumi na Uwekezaji Bwn. Mudrik Ramadhani Soraga na Abdalla Hussein Kombo Waziri wa uchumi wa bluu.

Wote kwa pamoja wamewahakikishia wawekezaji kuweka mazingira mazuri kwaajili ya kuwekeza, na serikali kuendelea kushirikiana na taaisi mbalimbali juu ya ajenda ya uchumi wa bluu na kukuza sekta ya uvuvi.

"Mipango mingi ya kimkakati inatekelezwa, tunataka watu makini na wenye uwezo wa kufanya kazi kufikia malengo, unganeni nasisi katika mipango ya uwekezaji iliyoidhinisha" amesema Waziri Kombo.

Katika sekta ya uvuvi pekee visiwani Zanzibar huchangia 2.6% ya pato ghafi la Zanzibar, hutoa ajira za moja kwa moja kwa watu 200,000 na zaidi ya watu laki 4 hutegemea sekta hiyo.