Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552514

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Serikali inakamilisha mifumo ulipaji wanufaika TASAF

TASAF kuwalipa wanufaika Kielekroniki. TASAF kuwalipa wanufaika Kielekroniki.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unakamilisha mpango wa kuingia kwenye mfumo wa kuwalipa ruzuku wanufaika kwa njia ya kielectroniki katika mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa na Mfuko huo.

Afis Ufuatiliaji Bi. Linna Marealle amesema utekelezaji wa kipindi cha awamu ya tatu ya TASAF wanufaika wote watalipwa ruzuku zao za kila mwezi kwa njia za kielekroniki kwa kutumia simu na akaunti za benki. Utaratibu huo unatofautiana na wa awali ambapo fedha zilikuwa zikiwafikia wanufaika zikiwa pungufu.

"Hata hivyo kwa baadhi ya wanufaika ambao hawana simu na akaunti za benki, tunakamilisha mpango wakukutana na wakala maalum ambao watawalipa ruzuku zao kila mwezi ili kila mmoja afurahie maisha akiwa kwenye makazi bora"

Bi. Marialle alieza kuwa utekelezaji wa mpango huo kwa mwaka 2021/2023 imewalipa kaya 1,450,000 kwa vijiji 6000 Tanzania Bara na Visiwani na tayari halmashauri 184 zimefikiwa.