Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559975

Habari za Afya of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kuboresha huduma za Afya hospitali za kanda na mikoa

Waziri wa Fedha  Dkt. Mwilgulu Nchemba Waziri wa Fedha Dkt. Mwilgulu Nchemba

Katika kukuza miundo mbinu bora ya Afya nchini Serikali imesema kuwa katika kila hospitali za zinapaswa kuwa na vipimo vyote vikubwa ndani ya miezi sita.

Waziri wa Fedha Dr Mwigulu Nchemba ameyasema hayo Septemba 26, wakati wa kilele cha maadhimisho ya maonesho ya Madini Mkoani Geita.

"Hospitali zote za mkoa zinapaswa kuwa na vipimo vyote ikiwemo CT-Scan ,Utrasound pamoja na X-ray" amesema Dr Mwigulu

Akizungumza maswala ya utoaji huduma za afya nchini, amesema Serikali inampango wa kuleta vipimo vya (MRI) katika hospitali zote za Kanda, lengo kuu likiwa ni kuimarisha huduma bora za afya .

Kufuatia chagamoto ya vipimo vya magonjwa makubwa madaktri hulazimika kuwambia wagonjwa waende hospitali kubwa za mjini ili kupata huduma hizo huku ikileta chagamoto kubwa kwa wananchi kutoka maeneo ya mbali kuja mjini kwa ajili ya matibabu.