Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558835

Habari za Mikoani of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kuchunguza vyama vya ushirika

Serikali kuchunguza vyama vya ushirika Serikali kuchunguza vyama vya ushirika

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atapeleka timu maalumu ya wataalamu mkoani Kagera itakayofuatilia uendeshaji wa vyama vya ushirika ili kujenga mfumo bora ndani ya vyama hivyo kwa manufaa ya wakulima wa Mkoa huo.

Amesema hayo akiwa Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera mara baada ya kuzindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo huku akitaka kufahamu namna vyama hivyo vinavyojiendesha na mfumo unaotumika katika mauzo ili kuondoa malalamiko ya wakulima katika malipo.

"Dosari zipo nyingi kwenye kahawa, kwanza nilete ukaguzi kwenye vyama vyote tuone namna wanavyoendesha, lakini tujue mali zilizopo kwenye vyama vikubwa vyote vya ushirika, kisha tuvitambue vyama vya msingi na namna vinavyo endeshwa tutawapa mfumo mzuri, niwape faraja wakulima kuwa tunakuja Serikali kuweka miguu miwili huku huku Kagera na tutapitia kila chama cha msingi na utaratibu wanaotumia" Waziri Mkuu

Ameongeza kusema kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia, imedhamiria kwa dhati kuwatumikia watanzania wote, na kuwa Rais Samia ametoa maelekezo kwa ambayo yanalenga kumjenga na kumnufaisha mtanzania.