Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585457

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali kufanya marekebisho sheria TCRA

Serikali kufanya marekebisho sheria TCRA Serikali kufanya marekebisho sheria TCRA

Serikali imesema itafanya marekebisho katika Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kutoa fursa kwa wasanii kupata matangazo kwenye tamthilia zao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa vipindi mbalimbali vya televisheni ikiwamo tamthilia. Alisema hayo baada ya mwigizaji mkongwe, Vicent Kigosi ‘Ray’ kuomba serikali kuwapa nafasi ya matangazo ya tamthilia zenye maudhui ya ndani kwa kuwa TCRA haijatoa fursa hiyo.

“Ni kweli kanuni za TCRA haziruhusu kuweka mambo fulani kama matangazo ila msiwe na wasiwasi, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iko tayari kuwasaidia, suala hilo limefanyiwa kazi,” alisema.

Alisema kanuni zijazo za mamlaka zitarekebishwa na kuwataka wasanii wasiwe na wasiwasi juu ya jambo hilo mambo yatakuwa mazuri baadaye. Wakati huo huo, Dk Abbasi alisema kila mwezi watakuwa na jambo jipya la kuwapa wasanii hivyo wakae mkao wa kula.