Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551143

Habari Kuu of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kuimarisha mawasiliano mipakani

Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Mhandisi Kundo Mathew Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Mhandisi Kundo Mathew

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imelenga kuimarisha huduma za mawasiliano katika maeneo yote ya mipakani Tanzania.

Haya yameelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Mhandisi Kundo Mathew, ambaye alieleza lengo la serikali kufanya hivyo ni kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kuongeza na kuinua uchumi wa nchi.

Kundo aliongeza kusema kuwa zipo fursa nyingi zinazopatikana mipakani hivyo mpango huu utaibua na kuimarisha uchumi wa wananchi waishio katika maeneo yote ya mipakani, lakini pia utapunguza matukio ya uhalifu yanayotokea katika ma Seneo hayo.

Wizara hiyo pia ipo katika hatua za kuhakikisha minara ya mawasiliano inayojengwa kuanzia sasa inakuwa na uwezo wa 3G na kuendelea pamoja na kuiboresha minara ya zamani iliyokuwa na uwezo wa 2G kwenda 3G na kuendelea ili kuhakikisha kunakuwa na mitandao yenye nguvu itakayowezesha kupatikana kwa huduma ya mawasiliano ya simu na intaneti