Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 20Article 558649

Habari Kuu of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kujenga madaraja 690 nchi nzima

Serikali kujenga madaraja 690 nchi nzima Serikali kujenga madaraja 690 nchi nzima

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema ndani ya mwaka huu serikali imejipanga kujenga madaraja 690 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ametoa kauli hiyo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa daraja linalojengwa chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijini (TARURA) wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 200.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa katika kuhakikisha miundombinu ya vijijini, serikali imeweza kuongeza bajeti ya TARURA kutoka shilingi milioni 275 hadi bilioni 940 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hivyo amewataka wananchi kutegemea mabadiliko makubwa katika kutatua kero za miundombinu ya barabara nchini .