Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541882

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali kujenga shule za sayansi za wasichana kuondoa pengo la kidigiti

Serikali kujenga shule za sayansi za wasichana kuondoa pengo la kidigiti Serikali kujenga shule za sayansi za wasichana kuondoa pengo la kidigiti

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema serikali inakusudia kuanzia Julai mwaka huu kujenga shule za sekondari za sayansi za watoto wa kike ili kuziba pengo la maendeleo ya kidigitali .

"Tutaanzisha shule za sekondari, lengo ni kuziba pengo la kidigitali. Kwani uchumi wa viwanda unahitaji makundi yote mawili, tuzibe pengo kidigitali."alisema na kuongeza;

“Katika maeneo mengi vijana wa kiume wamejiajiri vibandani lakini watoto wa kike wanafanya kazi ya kuuza nyanya na mchicha. Tuzibe pengo hilo kwa ajira ya watoto wa kike”.

Alisema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza na wanawake huku akisema kuwa, wanaume wana uwezo wa kuitumia mifumo hiyo kuliko wanawake na kutolea mfano wa wajukuu zake .

Kwa mujibu wa Rais Samia, Ibrahim mwenye umri wa miaka tisa kwenda 10 ana uwezo zaidi wa kutumia mifumo ya teknolojia kwenye simu kuliko Samia.

"Mimi nikikwama namwita mjukuu wangu Ibrahim aangalie simu yangu , anachukua simu akiangalia dakika chache anarudisha anakuambia ipo tayari,"alisema na kuongeza akipata changamoto kwenye simu akimpata Samia huwa hapati ufumbuzi

“Nikimwambia Samia mjukuu wangu chukua simu anasema mimi sijui ngoja nimwite Ibra."

Samia alisema wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi ukiwemo umbali kutoka mahali wanapoishi, uhaba madarasa, uhaba wa vyoo, maji hakuna na matatizo mengine ambayo yanawakumbana hivyo serikali inaendelea kujenga miundombinu ya elimu na anaamini shule hizo zitajengwa kwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ni mwanamke.

Rais Samia alisema katika kuboresha teknolojia, hata katika vyombo vya upatikanaji wa haki ikiwemo mahakama yamefanyika maboresho ikiwemo mifumo ya uendeshaji kesi.

“Jaji kiongozi nikimpigia simu, kesi ngapi zimehukumiwa, mchakato na zilizoisha kabisa, ataingia kwenye kompyuta anaangalia zamani angesema naomba wiki nikaangalie”alisema.

Join our Newsletter