Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559903

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kujenga vyumba 15,000 vya Madarasa

Rais Samia Hassan Suluhu Rais Samia Hassan Suluhu

Serikali imezungumzia swala la Elimu na Afya bora nchini ikiwa bado Serikali inaendelea na jitahadi za kutatua changamoto kwenye sekta hizo katika makazi ya Wananchi.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa viongozi wa ALAT mkoani Dodoma, Rais Samia amesema;

"Nimetoa maelekezo fedha tumayokusanya kwenye tozo ikajenge vituo vya afya na madarasa lakini nataka niwaambie kuna kafedha kingine nimekipata pahala tunakwenda kumaliza madarasa yote”

Aidha Rais Samia amesema aliambiwa swala la uhaba wa madarasa Elfu 11 lakini katika fedha walizopigia mahesabu zitajenga madarasa Elfu 15, ili kufikia Januari mwakani Watoto wote waingie shule pamoja.