Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 26Article 574138

Habari Kuu of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali kuongeza ndege tano ATCL

Serikali kuongeza ndege tano ATCL Serikali kuongeza ndege tano ATCL

Shirika la ndege la Tanzania, ATCL limesema kuwa linatarajia kuongeza ndege nyingine tano pamoja na kuongeza, kurudisha safari katika maeneo mengine ndani na nje ya Afrika.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL , Ladislaus Matindi mapema Novemba 26,2021 wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam -Nairobi.

Amesema kuwa wamejipanga kuongea safari hizo ili kukuza wigo wa biashara baina ya Tanzania na nchi za Afrika pamoja na zile za Ulaya, sambamba na hilo wamenuia kurejesha safari za China na Afrika Kusini.