Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540172

xxxxxxxxxxx of Thursday, 27 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Serikali kuruhusu kilimo cha bangi

Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Christina Rwehabuza, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya mpango kazi kwa ajili ya kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu dawa za kulevya.

Katika mafunzo hayo, Rwehabuza alisema kila wakati amekuwa akiulizwa maswali kuhusu kifungu cha 12 kama mamlaka imeshatengeneza kanuni za kuruhusu ulimaji wa bangi.

“Kifungu hicho ndiyo kimerekebishwa, kwa hiyo kanuni kuhusu kuruhusu bado hatujazitengeneza kwa sababu Umoja wa Mataifa (UN) wanaendelea kulifanyia kazi suala hilo waje watoe tamko ili nchi zote zitengenezewe miongozo,” alisema.

Alisema hata ikitokea wataruhusu ulimaji wa bangi, haitalimwa kiholela lazima wajiridhishe na kilimo hicho kitakuwa ni kwa ajili ya tiba na utafiti.

Akizungumzia sheria mwaka 2015 kama ilivyorekebishwa mwaka 2019 alisema imegawanyika sehemu saba na sehemu ya pili inazungumzia makatazo ya kujihusisha na dawa za kulevya.

Alitolea mfano endapo mmiliki wa ardhi akamkodisha mtu alime halafu akalima bangi, ikithibitika mmiliki atafungwa kifungo cha miaka mitano na kisichozidi miaka 30 na fani isiyopungua milioni tano au isiyozidi milioni 50.

Rwehabura alisema sheria ya dawa za kulevya inaelekeza utoaji wa adhabu ikiwamo kutumia, kuwezesha, kusafirisha na kumpangisha nyumba muuza dawa za kulevya.

“Ukikutwa na mitambo ya kutengeneza dawa za kulevya, adhabu yake ni jela maisha na faini ya Sh. milioni 200, kwa watumiaji faini yake ni isiyopungua Sh. milioni moja au jela miaka mitatu,” alisema.

Alisema kumpangisha muuzaji wa dawa za kulevya kwenye nyumba faini ni isiyopungua Sh. milioni tano, jela miaka mitano au isiyozidi miaka 30 au adhabu zote kwenda sambamba.

Alisema kwa wale wanaofadhili watu kufanya biashara hiyo adhabu ni jela maisha na faini ya Sh. bilioni moja.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya, alitaka wananchi na waandishi wa habari wawe na imani na mamlaka kwa sababu wana watumishi ambao wanawafuatilia siku hadi siku hivyo hakuna taarifa ya siri itakayotoka nje.

“Mapambano tumeyapa sura mpya, wote wanaojihusisha au kuwa na wazo la kutaka kujihusisha na dawa za kulevya ni vyema watafute biashara nyingine kwa sababu tunafanya kazi usiku na mchana kama ni kupumzika ni baada ya kufa, tunataka kizazi kisichotumia dawa za kulevya,” alisema.

Alisema waandishi wa habari wana nafasi kubwa kuieleza jamii dawa za kulevya zinapaswa kuchukiwa kwamba zinapotosha nguvukazi ya taifa.

Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka hiyo, Dk. Peter Mfisi, alisema mtumiaji wa dawa za kulevya yeyote mara anapotumia inaharibu mfumo wa fahamu wa binadamu na kwamba si kitu cha kufanyia mzaha.

Imeandaliwa na Romana Mallya na Hellen Mwango

Join our Newsletter