Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 09Article 556447

Habari Kuu of Thursday, 9 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali kusaini mikataba 1176 ya maji vijijini

Serikali kuingia mikataba 1176 ya maji vijijini Serikali kuingia mikataba 1176 ya maji vijijini

Serikali Kupitia Wizara ya Maji inatarajia kuingia mikataba wa jumla ya miradi 1176 ya maji vijijini kwa mwaka 2021/22 ili kuweza kutimiza adhma ya Rais Samia ya kumtua mama ndoo ya maji.

Taarifa hii imethibitishwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso, na kubainisha kuwa miradi 62 kati ya 177 iliyochukua muda mrefu kukamilishwa itakamilishwa ifikapo mwezi Desemba 2021.

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa Wizara hiyo iliweka mkakati wa kutekeleza Mradi huu kwa miji 28 nchini. mradi huu unatajwa kuwa na thamani ya Trilioni 1.2, huku akibainisha kuwa tayari mpango umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 47 tangu kuanzishwa kwake.