Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541261

xxxxxxxxxxx of Sunday, 6 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali mbioni kutekeleza mradi wa gesi asilia

WAZIRI Kassim Majaliwa amesema serikali ipo mbioni kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi utakaogharimu dola za Kimarekani bilioni 30.

Alisema mradi huo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amepania kutekeleza katika awamu ya sita na utakapoanza, utatumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka 25.

Alitoa taarifa hiyo jana wakati wa mkutano na wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Lindi.

“Vile viwanja mlivyovichukua anzeni kuvijenga, mradi wa gesi asilia unakuja, naamini mradi huu ukianza baada ya kukamilisha makubaliano, tutafika hatua nzuri” alisema.

Aidha, Majaliwa (pichani) alizitaka halmashauri nchini kuongeza usimamizi kwenye sekta ambazo wananchi wanazitekeleza kila siku ikiwamo ya kilimo na kuifanya moja ya ajenda muhimu kwa kuwa Watanzania wengi wanategemea kilimo katika kujipatia kipato.

“Halmashauri zetu nyingi watu wake ni wakulima, wafanyakazi ni asilimia tano tu na hata wafanyabishara ni asilimia ndogo, viongozi simamieni kilimo ili kiimarishe mapato ya mtu mmoja mmoja”

Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa Lindi kufanya kazi kwa bidii na weledi kuinua uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020/25 inaelekeza kuwa katika kujenga uchumi ni lazima uakisi maisha halisi ya kila siku ya wananchi na uwe shirikishi na shindani.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack alisema watahakikisha rasilimali zilizopo mkoani humo zinawanufaisha wanaLindi na Taifa kwa ujumla. “Tumekubaliana kwamba lindi ni tajiri, biashara zote

zinazofanyika kwasasa tunakwenda kuzitafsiri katika maisha ya watu wetu,” alisema.

Join our Newsletter