Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 26Article 544246

Habari za Afya of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yaanza kugawa vifaa vya maabara

Serikali yaanza kugawa vifaa vya maabara Serikali yaanza kugawa vifaa vya maabara

SERIKALI imeanza kugawa vifaa vya maabara kwa shule za sekondari na msingi na vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu nchini vyenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.4 wakati Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wakitakiwa kuhakikisha vifaa hivyo vinafi ka shuleni kabla ya Juni 15 mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi wa ugawaji na usambazaji wa vifaa hivyo leo jijini Dodoma, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),David Silinde alisema vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) na Mpango wa Kuimarisha Kusoma, Kuandika na Kuhesabu(Lens).

Alisema vifaa vya maabara vitagawanywa kwa shule za sekondari 1,253 na kutumika katika maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia na vifaa saidizi vitapelekwa katika shule 697 za msingi na sekondari ili kuimarisha uoni ,uwezo wa kujongea, usikivu, kujikinga na mionzi hatarishi ya jua kulingana na uleamvu wao. “Ununuzi wa vifaa hivi ni jitihada za serikali katika kuongeza ushiriki wenye tija kwa wanafunzi katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji. Pia makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi, ahakikisheni mnawasilisha taarifa ya mapokezi na usambazaji wa vifaa hivi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kabla ya Julai 20, mwaka huu,” alisema. Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leornad Akwilapo , alisema vifaa hivyo vimegaiwa ili kutoa fursa ya kupata elimu muda wote. Awali, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli alisema vifaa saidizi vinapelekwa katika hal mashauri 65 zenye vitengo na shule za mahitaji maalum ambazo hazikupata vifaa hivyo katika ugawaji wa awamu ya kwanza. Alisema ugawaji wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, ambayo pamoja na mambo mengine imeweka malengo ya kuwa na idadi ya kutosha ya wananchi walioelimika katika sayansi na teknolojia na hivyo kukidhi mahitaji ya maendeleo ya taifa.