Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541489

Habari Kuu ya

Chanzo: ippmedia.com

Serikali yahimiza uboreshaji mfumo ya huduma za mawasiliano

Serikali yahimiza uboreshaji mfumo ya huduma za mawasiliano Serikali yahimiza uboreshaji mfumo ya huduma za mawasiliano

Akizungumza wakati alipotembelea mifumo hiyo kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar Es salaam, , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine E. Ndugulile amesema wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.

“Upatikanaji wa huduma bora, za uhakika na salama ni jambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa” amesema Ndugulile.

Katika ziara hiyo Ndugulile alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabiri Bakari pamoja na Menejimenti.

Dk. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa kujenga mifumo wezeshi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano, ambapo alisema uboreshaji wake ni muhimu sana.

Baadhi ya mifumo aliyotembelea Waziri ni Mfumo wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT).  TZ-CERT pia akatoa ushauri wa kitaalam namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbalimbali ya Kimtandao kwa Taasisi na Kampuni mbalimbali hapa Nchini.Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BoT).Join our Newsletter