Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 22Article 559033

Habari za Afya of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yakabidhi magari 7 kusaidia huduma za Afya mikoani

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima leo Septemba 22, amekabidhi magari saba yatakayotumika katika shughuli za afya na mazingira na usafi katika mikoa mbalimbali.

Dk. Dorothy amesema, Wizara ya Afya inaendelea kutekekeza programu ya huduma endelevu za Maji na Usafi wa mazingira yenye lengo la uboreshaji miundo mbinu ya upatikanaji wa maji na huduma za Usafi wa mazingira vijijini.

Hata hivyo amesema, Program hiyo inatekelezwa kwenye mikoa 17 katika Halmashauri 86 nchini, mikoa iliyopokea magari hayo siku ya leo ni mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Simiyu Geita, Tabora, Katavi, Singida, Rukwa, Songwe, Iringa, Manyara, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

"Wizara itaendelea kuwezesha Halmashauri na Mikoa kutatua changamoto za usafiri kwa kadri itavyopata rasilimali fedha kupitia programu hii pamoja na kutenga fedha za kununua vyombo vya usafiri ambapo kwa mwaka huu wa fedha itanunua magari mengine 5 kwaajili ya Mikoa,” amesema Dk. Dorothy.