Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541501

Habari Kuu of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yakazania upatikanaji mbolea bei nafuu

Serikali yakazania upatikanaji mbolea bei nafuu Serikali yakazania upatikanaji mbolea bei nafuu

Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetakiwa kuanisha mkakati wa upatikanaji wa mbolea nchini kwa bei nafuu.

Waziri wa Kilimo, Preofesa Adolf Mkenda ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza kwenye kikao kazi alipotembelea taasisi hiyo kujionea hali ya utendaji na upatikanaji wa mbolea wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dar es salaam.

Pamoja na kuandaa mkakati wa urahisishaji wa upatikanaji wa mbolea, Pia Waziri Mkenda ameitaka taasisi hiyo kuandaa mkakati wa uanzishwaji wa viwanda vipya vya mbolea ili kuongeza uzalishaji wa pembejeo hiyo hapa hapa nchini.

Waziri Mkenda, amesema Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea, ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa uzalishaji wa ndani wa mbolea, unapewa kipaumbele na kwa kuongeza uanzishwaji wa viwanda vipya; mbolea itakuwa ikipatikana kwa urahisi, nafuu na kila Mkulima atamudu kuinunua na kuitumia.

Profesa Mkenda ameongeza kuwa Bodi na Menejimenti ya TFRA ibuni mkakati wa namna bora ya kuongeza uwekezaji hapa hapa nchini, kwa kuwa hilo ndiyo suluhisho la kweli katika kuwahakikishia Wakulima wengi wadogo unafuu bei.