Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573874

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Serikali yakiri ukosefu ajira kwa vijana, suluhisho lawekwa kapuni

Serikali yakiri ukosefu ajira kwa vijana, suluhisho lawekwa kapuni Serikali yakiri ukosefu ajira kwa vijana, suluhisho lawekwa kapuni

Suala la ajira limegeuka wimbo nchini, kila mwaka, kila awamu ya uongozi inazungumza kuhusu ajira na mara nyingi huzungumzwa katika upande mwingine wa shilingi yaani upande hasi.

Wahanga wa kuu wa panda shuka za ajira nchini ni vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 ambao wengi wao huwa kwenye hatari ya kukosa ajira kabisa.

Mapema hii leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizindua matokeo ya tathimini ya matokeo ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka 2020/2021 amesoma takwimu ya kuongezeka kwa ukosefu kwa ajira za vijana nchini kuwa hadi sasa ni asilimia 12.6 ya vijana hawana ajira.

Hali hiyo imeongezeka kutoka asilimia 12.1 ya mwaka 2014 hadi asilimia 12.6 kwa kipindi cha mwaka 2020/2021.

Kundi hilo la vijana ndio nguvu kazi ya taifa lolote lile hapa duniani, hivyo kushuka kwa kiwango cha ajira kunatishia ukuaji wa uchumi nchini.

Waziri Mkuu amesema kuwa katika asilimia hizo zilizowasilishwa na Tume hiyo, zinaonesha idadi kubwa ya vijana wa kike ambao kimsingi ndio waathirika wakubwa wa tatizo la ajira.

"Tunayo changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 15, ambapo kwa vijana wa kike ukosefu wa ajira upo kwa asilimia 16.7 na wa kiume ni 8.3...." Waziri Mkuu.

Aidha ripoti ya jumla inaonesha ukosefu wa ajira umepungua kwa asilimia 9.3 kwa mwaka 2020/2021 kutoka asilimia 10.3 ya mwaka 2014.

Hata hivyo Waziri Mkuu hakuweka bayana kuhusu mikakati ya Serikali katika kupambana na janga hilo ambalo ni tishio kwa taifa.