Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 08Article 541669

Habari Kuu of Tuesday, 8 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Serikali yalipa deni la trilioni 6.84-/

Serikali yalipa deni la trilioni 6.84-/ Serikali yalipa deni la trilioni 6.84-/

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mwingulu Nchemba, akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi Mwaka wa Fedha 2021/22, alisema deni la nje ni Sh. trilioni 2.74, ikijumuisha riba ya Sh. trilioni 0.63 na mtaji Sh. trilioni 2.11.

Alisema kazi nyingine zilizofanyika ili kudhibiti deni la serikali ni pamoja na kuhuisha mkakati wa muda wa kati wa usimamizi wa deni wenye lengo la kuendeleza soko la ndani la dhamana.

Pia, alisema kukamilisha mwongozo wa uandaaji wa miradi na utekelezaji wa Sheria ya mikopo, dhamana na misaada wa mwaka 2020 na kufanya tathmini ya uhimilivu wa deni Novemba mwaka jana, ambayo imeonyesha kuwa, viashiria vya deni la serikali vipo ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

Waziri Nchemba alisema katika kuimarisha usimamizi wa matumizi ya fedha za umma, wizara imeendelea kuzingatia taratibu za kutoa, kukagua, kufuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya serikali.

Waziri Nchemba alisema serikali imeendelea kufanya uhakiki na kulipa madai mbalimbali ya watumishi, makandarasi, washauri elekezi pamoja na fidia kwa miradi ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege na miradi ya maji.

“Hadi Aprili, mwaka huu, madai ya Sh. bilioni 965.1 yamehakikiwa na kulipwa, kati ya kiasi hicho, madai ya makandarasi ni Sh. bilioni 704.5, wazabuni Sh. bilioni 21.6, watumishi Sh. bilioni 97, madeni mengineyo Sh. bilioni 92.1, watoa huduma Sh. bilioni 34.2 na fidia kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ni Sh. billioni 15.7,” alisema.

Alisema katika mwaka 2020/21, washirika wa maendeleo waliahidi kuchangia katika bajeti ya serikali Sh. trilioni 2.8 na kati yake Sh. bilioni 949.32 ni misaada na Sh. bilioni 1,925.04 ni mikopo nafuu.

Alisema hadi Aprili, mwaka huu, washirika wa maendeleo wametoa Sh. trilioni 1.8, sawa na asilimia 70 ya makadirio ya kipindi hicho ya kuchangia Sh. trilioni 2.6.

Alisema kati ya kiasi hicho, misaada ya kibajeti ni Sh. bilioni 210.24, sawa na asilimia 100 ya makadirio ya kipindi hicho, miradi ya maendeleo Sh. trilioni 1.4, sawa na asilimia 64 ya makadirio ya Sh. trilioni 2.287 na mifuko ya kisekta Sh. bilioni 230.0, sawa na asilimia 87 ya makadirio ya Sh. bilioni 265.69 ya kipindi hicho.

Alisema katika mwaka 2020/21, wizara ilipanga kusimamia na kuratibu upatikanaji wa mikopo ya Sh. trilioni 4.9 kutoka katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti lakini hadi mwezi Aprili, mwaka huu, upatikanaji wake ni Sh. bilioni 3,992.71, sawa na asilimia 95.7 ya lengo la kokopa Sh. bilioni 4,170.01 katika kipindi hicho.

Alisema usimamizi madhubuti wa hatua za kodi na mikakati ya ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi umeiwezesha serikali kukusanya Sh. trilioni 16.95, sawa na asilimia 86.0 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 19.72 katika kipindi hicho.

Alisema kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yamefikia Sh. trilioni 14.54, sawa na asilimia 86.9 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 16.74, mapato yasiyo ya kodi kutoka kwenye wizara, idara zinazojitegemea, wakala na taasisi za serikali yamefikia Sh. trilioni 1.80, sawa na asilimia 78.5 ya lengo la kukusanya Sh. trilioni 2.30.

Join our Newsletter