Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 16Article 551722

Habari Kuu of Monday, 16 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yapiga STOP malipo ya Survey TANESCO

Shirika la Umeme Tanzania Shirika la Umeme Tanzania

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hakuna malipo yoyote ambayo Mtu anatakiwa kulipa kwenye huduma ya upimaji pale TANESCO wanapokwenda kuchukua vipimo kwa ajili ya kumuunganishia umeme (survey).

TANESCO wamesema iwapo itatokea Mfanyakazi wake yeyote akataka ulipie kuna namba wamezitoa ili Mtu apige haraka bila kuchelewesha muda ambazo ni 0768985100 au 0222194400.

“Endapo utaombwa kulipia hiyo huduma tunaomba kupata taarifa za Mfanyakazi wa TANESCO”

Tamko hili limekuja baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hususiani ni sula la kucheleweshewa huduma ya umeme kwa sababu ya kushindwa kulipia malipo hayo ambayo siyo halali