Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541846

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yapiga marufuku hospitali kuzuia maiti

RAIS Samia Suluhu Hassan amepiga mafuruku hospitali kuzuia maiti kwa sababu ya deni la gharama za matibabu.

Akizungumza na wanawake jijini Dodoma jana, Rais Samia alisema hakuna kudaia fedha wakati mgonjwa wamefariki, badala yake ni vyema gharama za tiba zikatolewa wakati mgonjwa akiendelea na matibabu.

“Wekeni mpango mzuri, hapa wananchi wanielewe, uwekwe mpango mzuri wa kulipa deni bila kuzuia maiti,” alisema Rais Samia na kuongeza kuwa mpango mzuri unaweza kuwa wa kutoa gharama za matibabu wakati mgonjwa anaendelea kutibiwa wala si kungoja hadi mgonjwa anakufa ndiyo unadai milioni tatu.

Alisema serikali imejitahidi kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati, lakini bado kuna pengo kubwa la watumishi, dawa na vifaa tiba na vitendanishi. Hata hivyo, alisema serikali imefanya juhudi kubwa kwani imesogeza huduma za afya vijijini na sasa asilimia 80 ya watoto wanazaliwa kwenye vituo.

“Tuongeze nguvu katika eneo hilo, tulisikia matatizo ya kutozwa huduma ya afya ya mama na mtoto, chanjo, vifaa vya kujifungulia na gharama za waliofariki,” alisema Rais Samia.

Pia alisema huduma za mama na watoto zitaendelea kuboreshwa kwani ana anajua kwenye matatizo hayo mawaziri ni wanamama. “Waziri wa Afya ni mama, yenye matatizo mawaziri ni mama, Tamisemi ni mama, Elimu ni mama. Wamama hawa wataenda kuchapa kazi na changamoto zitapungua,” alisema.

Kuhusu wanawake na mazingira, Rais Samia alisema shughuli za mazingira Tanzania “tumeanza kuharibu na maeneo mengine yameharibika kabisa, maeneo yenye vyanzo vya maji vimeharibika ndio maana tunapata tambua vyanzo.

“Twende tukashirikiane katika kutunza mazingira, vijijini na mijini miti na hewa, usafi mjini na vijijini,” alisema.

Join our Newsletter