Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541219

Habari Kuu of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yaruhusu balozi, taasisi za kimataifa kuingiza chanjo ya Covid-19

Serikali yaruhusu balozi, taasisi za kimataifa kuingiza chanjo ya Covid-19 Serikali yaruhusu balozi, taasisi za kimataifa kuingiza chanjo ya Covid-19

SERIKALI imeziruhusu Balozi na taasisi za kimataifa kuleta chanjo za ugonjwa wa Covid 19 kwa ajili ya kuchanja raia na watumishi wake .

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Rais Samia Suluhu Hassan amesema chanjo hizo zitaletwa kwa utaratibu utakaoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Rais Samia amesema Balozi na Taasisi zimeruhusiwa kuleta chanjo za ugonjwa wa corona…ili kuendana na taratibu za nchi zao na taasisi husika kuondoa kadhia wanazopata katika utendaji wa kazi zao kutokana na kutochanjwa,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha, Rais Samia amepokea mapendekezo ya mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa covid 19 na ya mapendekezo ya mpango wa kazi wa uratibu wa utoaji chanjo ya ugonjwa huo.

Mapendekezo hayo yaliwasilishwa jana Ikulu Chamwino mkoani Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya wataalamu aliyoiunda kwa ajili ya kushauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo, Profesa Said Aboud.

Katika mapendekezo hayo, kamati imeshauri njia mbalimbali zitakazowezesha serikali kupata fedha kutoka ndani ya bajeti ya serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwamo mashirika ya kimataifa na sekta binafsi kwa ajili ya kugharimia vifaa tiba, mafunzo na chanjo.

Samia aliipongeza kamati kwa kazi iliyofanya na akamuelekeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima kuandaa andiko litakalowasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa na baadaye serikali kufanya uamuzi mapendekezo yaliyotolewa na kamati.

Join our Newsletter