Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552262

Habari za Afya of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: ITV

Serikali yashauriwa kuingilia kati matatizo ya wataalam wa dawa

Chama cha Wafamasia Chama cha Wafamasia

Chama cha Wafamasia Tanzania kimeishauri serikali kuingilia kati matatizo yanayowakabili wataalamu wa dawa katika maeneo yao ya kazi na wamezishauri taasisi binafsi za kada ya afya kuona umuhimu wakuweka wataalamu waliobobea fani ya ufamasia katika taasisi zao kwa lengo la kutatua matatizo yasiyokuwa ya lazima yanayo lalamikiwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 18, katika kikao kazi cha wanataaluma wa kada ya famasi wa Mkoa Shinyanga walioko chini ya Baraza la Famasi Tanzania kilichofanyika Mkoani Shinyanga kwa lengo la kutoka na maazimio ya kuishauri serikali juu ya kuboresha na kupanua wigo wa wataalamu wa dawa nchini.

Kaimu Mganga wa Mkuu Mkoa wa Shinyanga, Bwana Timothy Sosoma ametoa angalizo kwa wafamasia hao licha ya wataalam wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kutaja matatizo kadhaa wana yokabiliana nayo katika kada ya ufamasia nchini.