Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 22Article 559114

Habari za Mikoani of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yasitisha huduma ya usafiri wa maji Kagera

Serikali yasitisha Huduma ya usafiri wa majini Kagera Serikali yasitisha Huduma ya usafiri wa majini Kagera

Serikali imesitisha utoaji wa huduma ya usafiri wa majini katika mkoa wa Kagera na Nansio wilayani Ukerewe mkoani Mwanza baada ya meli mbili za New Victoria Hapa Kazi Tu na New Butiama Hapa Kazi Tu kupandishwa kwenye chelezo ili kufanyiwa matengenezo.

Kaimu Mtendaji mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli, Mhandisi Abel Gwanafyo amesema meli hizo zimesitisha utoaji wa huduma ili kufanyiwa ukaguzi pamoja na matengenezo jambo ambalo ni utaratibu wa kawaida unaofanyika kila baada ya mwaka mmoja.

Amesema baada ya kufanyiwa matengenezo kitatolewa cheti cha ubora na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania Tasac.

New Victoria itasitisha huduma kwa siku 14 huku New Butiama hapa kazi tu itarejea baada ya siku nane.