Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541735

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yataka kampuni za simu kulinda siri za watumiaji simu

WAZIRI wa Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amezitaka kampuni za simu hapa nchini kushughulikia changamoto ya matumizi sahihi ya vifurushi na kuzuia uvujishaji wa siri za wateja.

Pia amesema Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) inatarajia kuitangaza zabuni ya kuepeleka Mawasiliano katika kata 179 zenye vijiji 358 Ikiwa Ni mkakati wa kupunguza changamoto za Mawasiliano kwa Wananchi waishio mipakani.

Dk Ndugulile ametoa rai hiyo alipozungumza na watendaji wakuu wa kampuni za simu katika kikao kilichokuwa na lengo la kujadiliana namna bora ya kupeleka mawasiliano katika maeneo ambayo hayana huduma ya mawasiliano.

Alisema anataka kuona kampuni hizo zinafanya uboreshaji katika hutoaji huduma na kushughulikia changamoto hizo.

" Mnatakiwa kuboresha huduma zenu hususani katika maeneo ambayo yanalalamikiwa na wananchi kama matumizi sahihi ya vifurushi pamoja na kukomesha tabia ya baadhi ya wafanyakazi wanaovujisha siri za wateja."

Aidha, Dk Ndugulile pia amezitaka kampuni za simu kuweka utaratibu wa kuwaaimamia mawakala wa kuuza laini za simu ili kudhibiti mawakala wasio waaminifu.

Join our Newsletter