Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 20Article 543526

Habari Kuu of Sunday, 20 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Serikali yatenga bilioni 62 kuweka umeme vijiji 384

Serikali yatenga bilioni 62 kuweka umeme vijiji 384 Serikali yatenga bilioni 62 kuweka umeme vijiji 384

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, wakati wa uzinduzi wa mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini kwa awamu ya tatu mzunguko wa pili mkoani humo, uliofanyika katika kijiji cha Namtumuka.

Amesema, kati ya vijiji 797 vilivyopo mkoani Mtwara, vijiji 413 tayari vimepatiwa umeme na vijiji vilivyosalia 384 vitapatiwa umeme katika Mradi huu ndani ya miezi 18 na hivyo kuweka historia ya mafanikio katika kutekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini.

Kalemani amesema itakapofika Desemba 2022, Tanzania itaandika historia katika vitabu vyake kuwa vijiji vyote vya Tanzania Bara vimepata umeme na kuungana na mataifa mengine duniani yaliyoendelea ambayo yameshaandika historia hii.

Hata hivyo amesema, hadi sasa, zaidi ya vijiji 10,312 vimeshapelekewa umeme na vilivyobakia takribani vijiji 1,956 ndivyo vinapelekewa umeme katika mradi huu.