Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 28Article 554167

Habari za Afya of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali yatenga bn 149/- kutekeleza bima ya afya kwa wote

Serikali yatenga bn 149/- kutekeleza bima ya afya kwa wote Serikali yatenga bn 149/- kutekeleza bima ya afya kwa wote

MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 149 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mpango wa Bima kwa wote.

Msigwa amesema serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Bima kwa Wote katika Kikao cha Bunge la Septemba mwaka huu na kwamba kiasi kilichotengwa ni cha awali na kitaanza kwa makundi maalumu.

“Huduma za mfuko wa bima ya afya zina umuhimu mkubwa katika jamii,” amesema Msigwa wakati wa Mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Wahariri unaofanyika jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu mfuko huo uanzishwe.

serikali yatenga bn 149/- kutekeleza bima ya afya kwa wote