Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 08Article 556018

Habari za Mikoani of Wednesday, 8 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Serikali yawahakikishia fidia walioathirika na kemikali za migodini

Serikali yawahakikishia fidia walioathirika na kemikali za Migodini Serikali yawahakikishia fidia walioathirika na kemikali za Migodini

Serikali imesema kuwa itaendelea kuhakikisha inasimamia taratibu zote za utunzaji wa mazingira katika migodi inayotiririsha maji yenye kemikali kwenye makazi ya watu ikiwa ni pamoja na kuwalipa fidia wle wote walioathirika na Kemikali hizo.

Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu waziri wa Wizara ya Madini, Prof Shukrani Manya, wakati akijibu swali la nyongeza liloulizwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Estar Bulaya, lililouliza, je ni lini Serikali itawafidia wananchi wanaoathirika na kemikali zinazotoka kwenye migodi.

Waziri Manya, amesema suala hilo linafanyiwa kazi ili kuhakikisha kuwa hakuna uchafu unaoendelea kutitirishwa kutoka katika migodi hiyo.

"Serikali imeendelea kufanya hatua, kuhakikisha hakuna maji yanayotiririshwa, timu yetu kwa kushirikiana na NEMC na idara ya maji, wameendelea kuhakikisha suala hili linazingatiwa"

Kuhusu kuwalipa fidia wanachi walioathirika na kemikali Waziri huyo amesema kuwa linafanyiwa kazi na mthaminishaji mkuu wa wa serikali.