Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559984

Uhalifu & Adhabu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Shahidi Kesi ya Mbowe Ahojiwa Matumizi ya Dawa za Kulevya

Shahidi Kesi ya Mbowe Ahojiwa Matumizi ya Dawa za Kulevya Shahidi Kesi ya Mbowe Ahojiwa Matumizi ya Dawa za Kulevya

SHAHIDI wa kwanza wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, amemaliza kujitetea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Shahidi huyo, Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo, ambaye kabla ya kufukuzwa kazi alikuwa ni komandoo wa JWTZ kikosi cha 92 KJ kilichopo Ngerengere, mkoani Morogoro.

Leo, Septemba 27, 2021 Kasekwa ameendelea kuhojiwa na upande wa mashtaka kuhusiana na ushahidi alioutoa mahakamani.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Kasekwa alitoa ushahidi wake kuhusiana na maelezo ya onyo ambayo aliyapinga kupokelewa mahakamani kama kielelezo kwa madai kuwa hakuyatoa kwa ridhaa yake, bali aliyatoa kwa kuteswa.

Maelezo hayo ya onyo aliyatoa kituo Kikuu Cha Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wakati akihojiwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, ACP Ramadhani Kingai, ambaye kwa sasa ni Kamanda ya wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

Kusekwa amehojiwa na Mawakili watatu waandamizi wa Serikali wakiongozwa na Robert Kidando, Nassoro Katuga na Abdallah Chaula, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Katika utetezi wake, Kasekwa amedai kuwa maelezo yake hakuyatoa kwa ridhaa yake mwenyewe, bali alitoa kwa kuteswa na kutishiwa.

Wakili Kidando na ameanza kwa kumhoji Kasekwa kwanini aliondolewa kazini?

Shahidi huyo amejibu kuwa aliondolewa kazini baada ya kupata tatizo la akili alilolipata baada ya kwenda vitani nchini Congo DRC, kulinda amani.

Wakili Kidando amemhoji shahidi huyo kuwa, kwa taarifa ambazo wanazo, Kasekwa alipelekwa hospitali ya Lugalo kutibiwa kutokana na kutumia dawa za kulevya.

Akijibu swali hilo, Kasweka amedai kuwa hajui.

Mbali na Kasekwa ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 16/2021, washtakiwa wengine ni Halfan Hassan, Mohamed Ling’wenya na Freeman Mbowe.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kigaidi.