Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559957

Uhalifu & Adhabu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: mwananchidigital

Shahidi kesi ya Mbowe adai kupigiwa simu na Luteni Urio

Shahidi  kesi ya Mbowe adai kupigiwa simu na Luteni Urio Shahidi kesi ya Mbowe adai kupigiwa simu na Luteni Urio

Shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, ameieleza Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jinsi alivyopigiwa simu ya kazi na Luteni Denis Urio wa Jeshi la Wananchi Tanzania ( JWTZ).

Shahidi huyo, Mohamed Ling'wenya amedai kuwa alipigiwa simu na Luteni Urio na kuelezwa kuwa amemtafutia kazi ya ulinzi kwa viongozi wakubwa yĆ ani ( VIP Protection).

Ling'wenya ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi ya ugaidi, ametoa ushahidi wake leo, Septemba 27, 2021 mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Ling'wenya anatoa ushahidi wake leo, kuhusiana na ushahidi alioutoa mshtakiwa Adam Kasekwa katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.

Soma hapa:Shahidi amedai kuwa alipata tatizo la akili, baada ya kwenda vitani Congo DRC

Kuwepo kwa kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kunatokana na mawakili wa upande wa utetezi kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adam Kasekwa, kutolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kama kielelezo katika kesi hiyo.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa utetezi, John Mallya, Ling'wenya amedai kuwa anamfahamu Adam kwa sababu walikuwa wote JWTZ kikosi cha 92KJ.

" Nakumbuka nikiwa Mtwara katika kampuni ya kusaga kokoto, nilipigiwa simu na Luteni Dens Urio na kuniambia kuwa amenitafutia kazi ya VIP Protection,( ulinzi wa viongozi)" amedai Ling'wenya na kuongeza.

" Baada ya simu ya Luteni Urio, nilimwambia baba na kisha waliongea kwa simu na Luteni Urio," amedai.

Shahidi huyo, ambaye aliajiriwa na JWTZ mwaka 2008 na kuachishwa kazi mwaka 2017, amedai Agosti 5, 2020 alienda Moshi kwa ajili ya kukutana na kiongozi wa Chadema, Freeman Mbowe kwa ajili mazungunzo ya kazi hiyo ya ulinzi.

Amedai akiwa Moshi, kabla ya kukutana na Mbowe alikamatwa na Polisi kisha kurejeshwa Dar es Salaam.

Mbali na Ling'wenya ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 16/2021, washtakiwa wengine ni Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Freeman Mbowe.