Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552430

Siasa of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Shaka apinga kufananisha siasa za Tanzania na Zambia

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamidu Shaka

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema uchaguzi wa Zambia ni tofauti na Tanzania kutokana na historia ya siasa nchini humo.

Shaka ameeleza utofauti huo uliojikita zaidi katika historia ya vyama vya siasa nchini zambia, hivyo uchaguzi huo hauwezi kuwa sawa na wa Tanzania kwakuwa chama kilichotolewa madarakani sio chama tawala.

"Niseme tu uchaguzi wa zambia ni tofauti na tanzania, ukifatilia historia ya zambia utajua, chama ambacho rais ametoka sio chama tawala, ni chama cha upinzani, chama ambacho kilitawala cha UNIP,kiliitawala zambia toka mwaka 1964-1991, ambacho ndio chama halali tangu mwaka 1972, kabla hakijaanguka ndio kikaingia chama cha NNPD.

Ametoa kauli hiyo, kufuatia gumzo lililoibuka katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakikihusiha Chama hicho na chama kilichotolewa madarakani,wengi wakitaka CCM kuiga mfano wa Zambia katika chaguzi za kisiasa.