Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 20Article 572932

Habari Kuu of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sheria ya ndoa ya 1971 kufumuliwa

Pro. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba Pro. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Serikali imepanga kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Rufani kwa kuandaa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kuhusu umri wa kuolewa.

Profesa Kabudi ameyasema hayo wakati akieleza mafanikio ya wizara yake katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Muswada huo amesema umepelekwa kamati ya Bunge kwa ajili ya kuupitia lakini iliurejesha serikalini ikitaka kuendelea kwa mashauriano na wadau.

Amesema wanaendelea kuwashirikisha wadau wengine kuona namna nzuri ya kutekeleza mahitaji ya watu ya umri wa kuolewa uwe kuanzia miaka 18.

Kuhusu uwakilishi wa mawakili, Profesa Kabudi alisema mahakama zote za mwanzo zenye mahakimu wenye shahada ya sheria mawakili wanaruhusiwa katika mashauri yao.

Amesema ndani ya mwaka mmoja mahakama za mwanzo zote nchini zitakuwa na mahakimu wenye shahada ili mawakili waweze kutumika.

Kuhusu kutafsiri sheria ziwe kwa Kiswahili, Profesa Kabudi alisema hadi sasa Sheria 154 zimetafsiriwa katika rasimu ya awali na mchakatochuo unaendelea kwa miaka miwili.

“Tunatumia rasimu ya kwanza ili sheria hizi zitumike baada ya hapo tukibaini maeneo yanayohitaji marekebisho tutafanya. Jambo kubwa ni kuwa na istilahi za kisheria kwa lugha ya Kiswahili,” amesema