Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540370

Siasa of Friday, 28 May 2021

Chanzo: ippmedia.com

Shigongo aona utashi kisiasa kuendeleza sekta mifugo, uvuvi

Shigongo aona utashi kisiasa kuendeleza sekta mifugo, uvuvi Shigongo aona utashi kisiasa kuendeleza sekta mifugo, uvuvi

Aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na uvuvi.

“Nimesoma sheria ya Uganda na Tanzania, ya kwetu iko kwa ajili ya kudhibiti na wenzetu ni kwa ajili ya kuwezesha, tukiendelea hivi tutabaki kukamata nyavu za wavuvi, kuzichoma bila mafanikio, inatakiwa nguvu iwe kwenye kuwezesha,”amesema. Kwa majibu wa Shigongo, Uganda ina Ziwa Victoria kwa asilimia 45 na uvuvi unachangia asilimia tisa ya pato la taifa, huku Tanzania yenye eneo kubwa ikichangia asilimia 12. 

Amesema samaki anatoa protini ya asilimi 20 huku Uganda ikiwa ni asilimia 50, huku ulaji wa samaki nchini humo mtu mmoja anakula kilo 15 hadi 20 na Tanzania ni kilo 5.5, kiwango ambacho ni kidogo. “Lazima tuamue kama nchi, watu wengi hawali samaki kutokana na bei kuwa kubwa, jimboni kwangu tuna wavuvi ila samaki ni ghali sana .Ili sekta ichangie uchumi wa nchi ni lazima kuwe na dhamira na kuachana na hofu bali tutende,”amesema.

Join our Newsletter