Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 22Article 559072

Habari za Mikoani of Wednesday, 22 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Shule iliyokatiwa maji kwa miaka mitano

Maji bomba Maji bomba

Wanafunzi 894 wa Shule ya Msingi Endiamtu wanalazimika kubeba Maji kutoka nyumbani kufuatia ukosefu wa hiyo shuleni hapo kwa takribani miaka mi tano na kupelekea hali ya usafi shuleni hapo kutorihisha.

Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule, Evetha Kyara amesema , Maji katika Shule hiyo yaliwekwa Mwaka 2010 lakini ilipofikia mwaka 2015 shule hiyo ilikatiwa maji ambapo hadi hivi sasa wanafunzi wanahangaika inawabidi watoke na maji kutoaka nyumbani.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani, Adam Kobelo amesema, hakuwa na taarifa yotote ya Maji kukatwa kwenye Shule hiyo .