Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552355

Habari Kuu of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Sikuagiza Gwajima Akamatwe"- Waziri Gwajima

Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Waziri wa Afya, Dk. Doroth Gwajima, amewataka watanzania kupuuza taarifa za uzushi zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwamba, ameagiza mbunge wa jimbo la Kawe Josephat Gwajima akamatwe kwa kupotosha umuhimu wa chanjo ya uviko 19.

Akiwa Jijini Mwanza amesema kupitia taarifa yake amelitaka jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), kumuhoji mbunge huyo kuhusu upotoshaji anaoutoa katika chanjo hiyo na si vinginevyo.

Vuta ni kuvute hii iliibuka tangu utoaji wa Chanjo ya Covid-19 kuanza nchini, hata hivo Waziri huyu alinukuliwa akisema kuwa amechoka kuvurugiwa Wizara kwa maneno ya upotoshaji yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.