Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552589

Uhalifu & Adhabu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Sikumbuki kushitakiwa kwa kujifanya Usalama wa Taifa" - Sabaya

Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, amedai hakumbuki kushtakiwa kwa kujifanya ofisa Usalama wa Taifa wala kuhojiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana, Sabaya alitoa madai hayo alipokuwa akihojiwa na mawakili wa Serikali, Tumaini Kweka, Felix Kwetukia na Baraka Mgaya kwa nyakati tofauti, kuhusu utetezi aliotoa mahakamani hapo.

Akihojiwa na Mgaya, Sabaya aliieleza mahakama kumtambua mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Sylvester Nyegu na kudai kuwa hakuwa msaidizi wake, bali alipangiwa kazi na mkurugenzi wa halmashauri ya Hai.