Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 10Article 546295

Habari Kuu of Saturday, 10 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Simbachawene ataka askari kuingia Dar City

Simbachawene ataka askari kuingia Dar City Simbachawene ataka askari kuingia Dar City

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameagiza familia 330 za askari polisi na maofisa 23 kuhamia kwenye nyumba za Mradi wa Dar City ambazo zipo wazi kwa miaka mitatu tangu zilipokamilika.

Simbachawene alitoa agizo hilo alipotembelea mradi huo ambao alisema tatizo imetokea baada ya serikali kubadilisha sera na kuzuia uwekezaji katika maeneo ya majeshi kupitia sekta binafsi. Mabadiliko hayo yalisababisha mkataba huo usiendelee.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo, sasa nyumba hizo zimebaki kuwa za polisi kwa sababu eneo hilo ni la polisi.

"Sasa kama hatuishi kwa sababu mkataba umesitishwa tunaendelea kupata hasara. Hili halina uhusiano na maelewano yoyote yanayoendelea kati ya mwekezaji na Jeshi la Polisi au serikali kuu,” alisema.

Aliendelea, "Nimesikia mlichosema kuhusu mradi huu wa Dar City ambapo kimsingi mradi huu chanzo chake ni kuboresha Jeshi la Polisi ambalo lilikuwa na dhamira ya kujenga makazi lakini pia linahusisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Osyerbay chenye ghorofa mbili ambacho nacho ni sehemu ya mradi huu lakini pia nyumba nyingine 23 pale Mikocheni za maofisa."

Alisema askari walihamishwa katika eneo hilo na kuhamishiwa uraiani wakati mradi huo ulipoanza na walilipiwa kwa miezi sita mara tatu, kisha wameendelea kujilipia hadi sasa.

Alisema kama waziri mwenye dhamana, ataangalia namna ya kumaliza mkataba huo na mwekezaji ili askari waingie kwenye nyumba hizo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro alisema mradi huo ulipoanza kujengwa askari wengi walikwenda kupanga uraiani lakini sasa muda wa kukaa huko umekwisha inabidi warudi kwenye nyumba hizo.

"Ninachojua Rais analishughulikia aliniambia nivute subira kuona maamuzi gani atayafanya kwa faida ya serikali na askari kwa ujumla," alisema na kumuomba Waziri awape maelekezo kwa kuwa wameshajipanga kuhamia kwa kujiwekea mpango wa kukaa.