Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584839

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Simiyu: Gari la Wanahabari Lagongana na Hiache, 11 Wafariki

Simiyu: Gari la Wanahabari Lagongana na Hiache, 11 Wafariki Simiyu: Gari la Wanahabari Lagongana na Hiache, 11 Wafariki

WATU 11 wamepoteza maisha wakiwemo wanahabari watano na abiria wa kawaida katika ajali iliyohusisha magari mawili ikiwa moja ni la abiria aina ya Toyota Hiace  na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara kugongana uso kwa uso leo Jumanne 11, 2022.


Taarifa za awali zilizotolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko imeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika Wialaya ya Busega, Simiyu na kwamba waandishi wa habari watano wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
 

Taarifa za awali

Gari la waandishi wetu wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega lilikuwa linaelekea Ukerewe kwa kupitia Bunda.

Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ng. Gabriel amethibitisha kutokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.

Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia. Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.

Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo.

Edwin Soko
Mwenyekiti
Mwanza Press Club
11.01.2022.


===================

Updates

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu 11 wamepoteza maisha huku wengine wakiwa katika hali mbaya ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu.