Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559918

Siasa of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Sintofahamu yaibuka kuelekea mkutano wa Msajili na TCD

Sintofahamu yatanda kuelekea mkutano wa Msajili na TCD Sintofahamu yatanda kuelekea mkutano wa Msajili na TCD

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPPs) na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) wanatakiwa kukubaliana juu ya jinsi ya kusuluhisha masuala ya kisiasa yanayoendelea kufuatia sintofahamu iliyopo baina ya vyama vya siasa pamoja na Jeshi la Polisi nchini.

Hata hivyo ofisi ya Msajili wa vyama imetangaza kukutana na vyama vya siasa pamoja na jeshi la Polisi kujadili tofauti zilizopo baina ya pande hizo mbili, huku ikinuia kukutana na kituo hicho cha demokrasia kwa ajili ya kujadili kuhusu masuala ya amani, haki pamoja na maridhiano kwa pande zote.

Kikao hicho kimepangwa kufanyika jijini Dodoma, huku Rais Samia akiwa mgeni rasmi na Makamu wa Rais wa Zanzibar, Othaman Masoud Othaman, akitarajiwa kuhitimisha kikao hicho.

Bado hatua hii ni kitendawili kwani vyama vya siasa hasa vya upinzani, vimeonesha kukata wito wa Msajili na mapema hii leo chama cha ACT-Wazalendo kimetoa tamko la kuungana na vyama vingine kutoshiriki kikao hicho.

Aidha Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini, Zitto Kabwe, ndiye kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, je hali hii ya kususia kikao cha Msajili wa vyama kinatoa taswira ipi katika kikao hiki cha TCD na ORPPs? mwarobaini wa vuta ni kuvute hii bain aya Polisi na Vyama ni ipi?.